TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 15 June 2012

Mtu mmoja ajiua kwa sumu ya panya


Na Mwandishi wetu

MKAZI  wa Mbagala aliyetambulika kwa jina moja la Shaibu (35) amekutwa amekufa chumbani kwake baada ya kunywa sumu ya panya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Temeke David Misime alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi jioni katika eneo la Mbagala baada ya polisi kukutwa mwili wa marehemu.

Alisema kuwa maiti hiyo ilikutwa imelala chumbani kwake ikiwa haina jeraha sehemu yoyote huku kukiwa na  matapishi pembeni.

Misime alisema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa  marehemu alikunywa  sumu ya panya na chanzo cha kujiua hakijafahamika kwasababu  marehemu hakuacha ujumbe wowote

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa  katika Hospitali ya Temeke kwaajili ya uchunguzi zaidi.

Katika hatua nyingine, mkazi wa Boko, Salum Said (19) amekufa baada ya kuzidiwa na maji wakati akiogelea katika ufukwe wa bahari ya Hindi.

Misime alisema, tukio hilo lilitokea juzi mchana wakati Said akiwa anaogelea
na mwili wake uliopolewa na  Askari wa zima moto wakishirikiana na Askari polisi na umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke .

Wakati huo huo, mtembea kwa miguu asiye fahamika jina  alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari katika barabara ya Mandela.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi mchana na kuhusisha gari aina ya Toyota Rav4 yanye namba T568 AVL .

Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na  Fadhili Kazia (35) likitoka maeneo ya buguruni kwenda Ubungo  lilimgonga mtembea kwa miguu na alikufa papo hapo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Amana


No comments:

Post a Comment