TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 28 June 2012

MH. MOHAMMED DEWJI AZINDUA KISIMA CHA MAJI



Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Gullam Dewji, ametumia zaidi ya shilingi milioni 22 kugharamia uchimbaji wa kisima kirefu cha maji cha kitongoji cha Mtisi, kata ya Mtamaa.

Dewji ambaye pia ni mjumbe wa NEC mkoa wa Singida, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima hicho, Alisema fedha hizo zimetumika pamoja na mambo mengine katika utafiti wa eneo lenye maji,uchimbaji  na ununuzi wa pampu ya mkono.

“Hapa naomba niweke mambo wazi, gharama hii inajumuisha pia uchimbaji wa kisima ambacho kwa bahati mbaya baada ya uchimba kina kirefu sana,kikawa hakina maji.  Pamoja na kukosekana huko kwa maji, lakini fedha nyingi zilitumika”,alifafanua.

Dewji alisema ameamua kutumia fedha zake binafsi kugharamia uchimbaji huo wa kisima, kwa lengo la kuwapatia maji safi na salama wakazi wa kata ya Mtamaa.

“Mimi binafsi naamini kwamba maji safi na salama, yatasaidia kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko ikiwemo, ugonjwa wa kuharaa”,alisema.

Aidha, mbunge huyo aliwataka wakazi wa kijiji cha Mtamaa na vijiji jirani, kukitunza kisima hicho ili kiweze kutoa huduma endelevu.

Dewji alisema kazi ya uchimbaji wa  visima, ni ya gharama kubwa mno, hivyo ni muhimu kisima hicho kikatuzwa  vizuri na kila mkazi wa eneo hilo, awe mlinzi ili kisiharibiwe.

Awali diwani wa kata ya Mtamaa (CCM) Mbua Chima, alitumia fursa hiyo kumshukuru mbunge Dewji, kwa msaada wa kuwachimbia kisima wakazi wa kata hiyo. 

Kwa hisani ya Mo blogu

No comments:

Post a Comment