TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 28 June 2012

SERIKALI KUTOA HUDUMA ZA MAJI


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

WIZARA ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar imesema lengo la serikali ni kuwafikishia huduma za maji wananchi wote wa Unguja na Pemba.

Naibu waziri wa wizara hiyo Haji Mwadini Makame aliwaambiwa wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu masuala katika kikao cha baraza hilo kufuatia suali la msingi lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe (CCM) Abdi Mosi Kombo aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi katika suala la kutatua kero ya upatikanaji wa maji.

Naibu waziri huyo alisema serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji kwa wakati muafaka na kuahidi kwamba meli ya waya na vifaa hivi karibuni itawasili katika bandari ya dar es salaam.

Awali Kombo alisema tatizo la maji kwenye jimbo la Matemwe kutokana na kisima kidogo Matemwe ambacho hakina uwezo wa kupandisha maji na kuwasaidia wananchi wa kijiji hicho na kuhoji ni lini serikali itawapatia wananchi wake mashine kubwa ili kuweza kupata huduma hiyo.

Akijibu suali hilo naibu huyo alisema uingiaji wa pampu siku zote unakwenda sambamba na uwezo wa kisima ulichonacho ambacho hutokezea dharura mafundi huweka pampu ndogo ndogo kwa muda wa kuhofia kuwakosesha wananchi huduma hiyo muhimu.

Alisema baada ya hapo hurejesha pampu ambayo inaenda sambamba na uwezo wa kisima kilichopo na kwa sasa tayari kisima cha kiachange kishawekewa pampu ambayo inakwenda sambamba na uwezo wa kisima na hivi sasa maji yanapatikana hadi kigomeni.

Akijibu ni sababu zipi zinzofanya mashine hiyo iunguwe mara kwa mara Naibu alisema “Sababu hasa zinazopelekea kuungua kwa mashine hizi ni hitilafu za umeme ikiwemo umeme mdogo ‘low voltage’ katika eneo hilo ambapo tayari ZAWA kwa kushirikiana na ZECO inafanya jithada kulitatua tatizo hilo” alisema.

SOURCE:Swahilivilla

No comments:

Post a Comment