TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 25 June 2012

Yakubu kufuata nyayo za Drogba


Straika wa Nigeria Yakubu ameamua kuiacha timu ya mpira ya  Blackburn baada ya kujiunga na Club ya  Guangzhou ya China.

Mchezaji huyo ambaye alishinda magoli 17 akiwa na timu ya Blackburn katika msimu uliopita  wa ligi  Ulaya tayari wameshajadili  mpango mzima wa kuhamia katika Club ya Guangzhou.
 
Mwezi Mei mwaka huu Yakubu alikuwa akitafuta  nafasi baada ya timu yake ya  kushuka daraja.
Ripoti ya dili hilo haijawekwa wazi ingawa inadaiwa kuwa atalipwa dola milioni 9.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka  29 atafuata nyayo za  Didier Drogba baada ya kuhamia China katika timu ya Shanghai Shenghua wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment