TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 16 July 2012

Nkosazana Dlamini-Zuma achaguliwa kiongozi wa kwanza mwanamke wa Au


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini amechaguliwa kuwa Kiongozi wa kwanza mwanamke wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika  AU.

Uteuzi huo umemaliza vutano katika kinyang’anyiro cha uongozi ambao ulikuwa umetishia kuugawanya na kuudhoofisha Umoja huo.

Kulikuwa na shangwe katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa baada ya Zuma, ambaye ni mke wa zamani wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kumshinda kiongozi anayeondoka Jean Ping wa Gabon.

Bibi Dlamini-Zuma aliungwa mkono na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, naye Ping akipigiwa sauti na nchi za bara Afrika zinazotumia lugha ya Kifaransa. 

SOURCE. Mo Blog

No comments:

Post a Comment