Mashabiki wanajitokeza kwa idadi kubwa mwaka huu kuangalia mechi za Ligi Kuu ya Kenya. [Tony Karumba/AFP]
Katika miaka ya karibuni, mahudhurio yamekuwa ya chini huku mechi
zikiangaliwa na watu wachache tu. Lakini tangu mwaka jana, ligi
imeshuhudia ongezeko la mahudhurio kwa sababu ya kile ambacho wengine
wanasema ni kutokana na mipangilio mizuri na ufadhili.
"Nimekuwa nikihudhuria mechi za mpira wa miguu ili kuangalia timu yangu
maarufu ya AFC Leopards kwa sababu ligi sasa imeandaliwa vizuri," Oscar
Kwena, mwenye umri wa miaka 46, aliiambia Sabahi.
Kwena, mkazi wa Nairobi, alisema kuwa anajua atafaidi thamani ya pesa
zake wakati anapokwenda kiwanjani kuangalia timu ake, ambayo kwa sasa ni
ya pili katika ligi.
Ligi haiwavutii wanaume tu; wanawake pia wanahudhuria kwa idadi kubwa.
"Ninahakikisha kuwa ninaangalia kila mchezo wakati wowote timu yangu
inacheza mechi zake mjini Nairobi," alisema Emily Okindi, msichana
mwenye umri wa miaka 22 na mfuasi wa Gor Mahia.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) huko Nairobi
Magharibi Simon Mugo aliiambia Sabahi kuwa ligi imepata umaarufu upya
kwa sababu ya mpangilio wake mzuri na ufadhili bora zaidi wa timu.
"Ufadhili wa timu tano za juu katika ligi kutoka kwa mashirika kumeipa
msukumo. Sasa tuna mechi zinazooneshwa moja kwa moja na DStv," alisema.
Timu za juu zimepata ufadhili kutoka makampuni makubwa. AFC inafadhiliwa
na Kampuni ya Sukari ya Mumias, Gor Mahia na Kiwanda cha Maziwa cha
Broookside Dairy na Sofapaka inafadhiliwa na Kampuni ya Saruji ya East
African Portland.
Tiketi kwa mechi nyingi zinauzwa kwa shilingi 500 (dola 6.2) kwa viti
vya VIP na shilingi 200 (dola 2.5) kwa viti vya kawaida. Uwanja wa Nyayo
ambako mechi nyingi huchezwa, una uwezo wa kuchukua watu 30,000.
Sehemu ulipo uwanja huo. kilomita tatu kutoka katikati ya mji, na
usalama ulioimarika wakati wa mechi, pia kumesaidia ongezeko la
mahudhurio mchezoni, Mugo alisema.
"Siku zimepita ambao urushaji mawe ulikua jambo la kawaida katika mechi
za mpira wa miguu," Mugo alisema, na kuongeza kuwa FKF inafanya kazi na
polisi ili kuimarisha usalama katika viwanja vyote.
Ufadhili bora zaidi pia umepelekea kuwepo na wachezaji bora zaidi na
kutangazwa zaidi na vyombo vya habari, alisema Robin Toskin, mwandishi
wa habari wa michezo anayeandikia gazeti ya Standard Group.
"Ubora wa mpira wa miguu ni mkubwa zaidi kwa sababu tuna wachezaji wazuri katika ligi," aliiambia Sabahi.
Mechi za ubora wa juu zaidi na makundi makubwa ya watu pia kumesaidia kuongeza ushindani miongoni mwa timu na wapenzi, alisema.
Miaka kumi iliyopita, timu za AFC Leopards na Gor Mahia zilikuwa hazina
ufadhili na mechi zao zingeweza kuvutia watu kidogo si zaidi ya 100,
Toskin alisema. Kinyume chake, mechi iliyochezwa na timu hizo mbili
tarehe 22 Septemba katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi uliwavutia watu
25,000.
Wafadhili sasa wanazivutia familia nzima, kutafutia soko mpira wa miguu
kama shughuli ya furaha kwa familia na kutoa burudani katika kabumbu ili
kuwavutia vijana, alisema.
Kuna mizunguko minne iliyobakia katika Ligi Kuu na mwisho wa msimu
unakaribia kukamilika. Ushindani mkuu ni baina ya timu zinazoongoza sasa
za Tusker, AFC Leopards, Gor Mahia na Ulinzi Stars.
"Wakati ligi inakaribia kumalizika, tutashuhudia wapenzi wengi
wakimiminikia viwanjani ili kuunga mkono timu zao kwa vile kombe sasa
lipo tayari kunyakuliwa," Toskin alisema.
Chanzo: sabahionline.com/
No comments:
Post a Comment