TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 21 November 2012

Mkereketwa: CCM wameiga sera za Chadema

Katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Novemba 10, 2010 katika Kata ya Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, nawakumbusha Watanzania wote na tegeni macho na masikio yenu, Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa alisema nanukuu “Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure” na kwamba lazima wananchi wachangie. Narudia tena “Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure” na kwamba lazima wananchi wachangie. Kaeni sawa maana narudia tena “Serikali haiwezi kutoa huduma za jamii bure” na kwamba lazima wananchi wachangie. 

Naendelea kunukuu usemi wa Mwenyekiti wa CCM Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete “Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu hiyo sera ya bure tulijaribu na ikatushinda na wakati huo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona hilo haliwezekani tukaamua tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa Elimu bure.” Mbona nyie wote mlisomeshwa bure mnachopinga ni kitu gani jamani nyie vihiyo wa CCM. 

Kwa upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika moja ya mikutano yake alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya elimu bure hadi sekondari kutokana na kulea Wezi, Wabadhirifu na kuthamini anasa kuliko maendeleo kwa wananchi. Leo hii wameona Watanzania wamejua na kushuhudia wanaibiwa Kodi zao, Madini yao, Wanyama wao, Misitu yao, Samaki wao, Ardhi yao, Ndugu Nape Mnauye anataka kudanganya umma wa Watanzania tena wasomi kuliko yeye kuwa eti “ELIMU BURE” ni sera ya chama chake cha CCM. Hivi huwaga nyie CCM mnapotoa matamshi yenu huwa hamrudii kuzisoma hotuba zenu mliziwahi kutoa kwa Watanzania.


CCM mkitaka msimame kwenye majukwaa hapa Tanzania na watu wawaamini sasa hivi kama wanavyoweaamini CHADEMA inabidi mrudishe kwanza mali za umma mlizikwiba, fedha za umma mlizoficha ulaya, mfute mikataba ya hovyo kabisa ya madini mliyowekeana na wawekezaji, muwatoe Wazungu wote mliowamilikisha ardhi ya Watanzania, Muwafukuze wawekezaji wote mliowapa vitalu vya kuua na kuuza wanyam wetu, na mrudishe elimu ya Watanzania iwe sawa kwa wote. Kwa kifupi mkubali kuwa masikini kama walivyo Watanzania.

Kusema kweli nyie CCM sasa hivi kushindana na CHADEMA ni ndoto za Alinacha au Abunuasi. Watanzania hawana imani na nyie tena. Kama kwenye uchaguzi wenu tu wa chama mnatumia mabilioni kuhonga nani anawaamini tena kuwakabidhi nchi. Kama mnawavunjia watu nyumba zao na kuwaacha wanalala nje nani tena ana imani na nyie. Kama mnawauzia hata wagonjwa wa ukimwi dawa bandia nani ana imani na nyie tena. Kama fedha za misaada ndizo mnaingiza kwenye uchaguzi na kuzitumia kwa rushwa nani tena anawaamini. Anayeiamini CCM sasa hivi ana kasoro za akili. Aende akapime Mirembe.

Mwisho na kila Mtanzania anielewe. CCM wakitaka Watanzania wawaamini warudishe mali zote za umma wanazomiliki na wahakikishe wanajitoa kwenye biashara wanazofanya na wawekezaji. Viongozi wa CCM ndio wauza mafuta, Viongozi wa CCM ndio wenye Mabenki, Viongozi wa CCM ndio wenye mahoteli makubwa makubwa, Viongozi wa CCM ndio wenye mashamba makubwa makubwa, Viongozi wa CCM ndio wenye mashamba ya mifugo, Viongozi wa CCM ndio wenye makampuni ya kuagiza magari, Viongozi wa CCM ndio wenye viwanda vikubwa vikubwa. Viongozi wa CCM ndio waliowadanganya Watanzania kuwa Serekali haiwezi kufanya biashara ili wafanye wao. Wakadiriki kuviua viwanda vyote nchini kikiwepo cha Matairi kule Arusha. Mimi nilishangaa. Magari yalivyo mengi Tanzania unadiriki kukiua kiwanda uagize tairi Kenya.

Eee Uwiiiiiii, narudia tena Watanzania Eeeeee Uwiiiiiiii Rushwa, Rushwa, Rushwa haitatoka Tanzania bila kukitoa chama tawala cha CCM madarakani. Misaada inakuja toka nje haiwafikii Watanzania kisa eti wanakiimarisha chama kishinde uchaguzi mwaka 2015. CCM wako madarakani kuhakikisha wanashinda kwenye chaguzi mbalimbali lakini sio kuhudumia Watanzania. Mimi nawaambia CCM sasa hivi Tanzania hakuna mjinga. Tena mahali mliharibu kuwekana nyie na wake zenu, na watoto wenu madarakani. CHADEMA tunawapa kura za “NDIO” mwaka 2015 nchi nzima na zungukeni kuwaamsha Watanzania wanaosubiri kupata maisha bora wakiwa ndani ya CCM. Msibishane majukwaani wala bungeni na hawa wajinga tangazeni sera zenu muwakomboe Watanzania kama alivyofanya Kamanda Robert Mugabe wa Zimbabwe. Ukitegemea kupata maisha bora ukiwa chini ya utawala wa CCM utasubiri sana.

Mkereketwa
Lengai Ole Letipipi

No comments:

Post a Comment