TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 21 November 2012

Wadau wa Afya wakutana jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kuboresha utoaji huduma za afya nchini

Mkurugenzi wa mafunzo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Mutahyabarwa Gozibert (katikati) akizindua kitabu cha mwongozo wa utoaji wa huduma bora za afya nchini kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika mkutano uliowahusisha wadau wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam(Picha na Aron Msigwa MAELEZO).
Mganga mkuu wa serikali mstaafu Dkt. Gabriel Mpunda akiwasilisha mada kuhusu mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma bora za afya nchini kwa wadau wa afya waliohudhuria mkutano wa taifa wa majadiliano ya utoaji wa huduma Bora za afya leo jijini Dar es salaam(Picha na Aron Msigwa MAELEZO).
Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Magreth Muhando akizungumza na wadau wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo kuhusu hatua zinazochuliwa kuboresha huduma za afya na uboreshaji wa elimu katika vyuo vya sayansi ya afya na tiba wakati wa mkutano huo  leo jijini Dar es salaam(Picha na Aron Msigwa  MAELEZO)

Wadau wa huduma za afya kutoka maeneo mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano huo(.Picha na Aron Msigwa  MAELEZO)

No comments:

Post a Comment