TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 12 December 2012

La moyoni

Katika mambo yaliyonikera ni siku ya tarehe 06/12/2012 wakati timu ya mkoa wa Dar es salaam inayojulikana kama Kilimanjaro Star ilipofungwa bao 3 bila na timu ya Taifa ya Uganda. Hiyo ni aibu ya TFF, Ikulu na Mkuu wa mkoa Wa Dar es salaam. “REST IN PEACE TANZANIA”. Hayo yalikuwa maneno ya kejeli yameandikwa kwenye mabango ya mashabiki wa Uganda. Nchi isiyo ratiba ya maisha ya watu wake. Nchi inayoongozwa na kuendeshwa kisiasa bila elimu. Eti John Bokko, Idd Chuji, hawa ni masanamu tu uwanjani. Chujeni timu ya Taifa kwa kuchukua wachezaji timu za mikoani. Hawa wachezaji wanajisikia sana kuona kila mwaka wanachaguliwa wao kumbe hata viwango hawana.

 Wachezaji wameishia darasa la saba na labda kwa bahati wengine darasa na 10 na 14 la kufeli lakini wanafundishwa na Mzungu. Wachezaji wala Unga, Wavuta bangi, nidhamu hawana, kocha kasimama tu kama kanyeshewa na mvua. Wachezaji wanajua kabisa uwezo wa wafungaji wa Uganda lakini wanagongeana mpira maeneo ya golini kwao badala ya kupiga mpira mbele. Wachezaji Wazee, wachovu, wavivu, wazembe, afya mbovu eti wanaitwa wachezaji wa Taifa. Msitudhalilishe watu wa mikoani. Hii ni timu ya Dar es salaam.

 Kama ilivyo Serekali legelege hata katika michezo nchi hii ni legelege. Tanzania kila kitu Siasa. Kuanzia kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna, kula, na hata kwenda haja siasa tu. Kujifanya wakarimu huku kila kitu kinaenda shaghala baghala. CHADEMA chukueni nchi mrudishe heshima ya Taifa la Tanzania aliyoianzisha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kuonge bila matendo ni unafiki.

 Mwisho lakini halihusiani na michezo lakini lina umuhimu mkubwa sana. Trafiki Arusha wametuchosha na rushwa. Wanamiliki majumba makubwa ya kifahari kule kwa mrombo na wanaongoza kwa kuwa na magari mengi mabovu ya abiria. Serekali tusaidieni kuwahamisha askari hawa wala rushwa. Kinachochangia watu wa Arusha kuichukia CCM ni hawa askari wa trafiki barabarani. Wanakamata magari mapya ya watu binafsi na kuchukua rushwa wakajenge kwa Mrombo lakini magari yao mabovu yanafanya kazi. Bila kuwahamisha hawa trafiki CCM mnajisumbua mkoa wa Arusha.

Mkereketwa

Gillard David

No comments:

Post a Comment