TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday, 2 January 2013

Sajuki ameaga dunia

Mwigizaji wa Filamu  Sajuki amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya hali yake kubadilika kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu, Sajuki alikuwa amelazwa katika dodi ya Mwaisela akipigania maisha yake katika hospitali hiyo.
Msanii huyo ameugua muda mrefu ambapo aliwahi kwenda India kutibiwa

 nchini India na baada ya kurejea kutoka mhuko afya yake iliimarika mpaka alipodondoka jukwaani tena katika tamasha la Bongo Movie jijini Arusha hivi karibuni.
Fullshangweblog imeongea kwa simu na mmoja wa wanafamilia ambaye amesema k

wa sasa shughuli za kuhifadhi mwili wa marehemu Sajuki  katika hospitali ya taifa ya Muhimbili zainaendelea na ndugu kadhaa wamekusanyika nyumbani kwake Tabata ambapo taarifa kamili za wapi msiba utakuwa na mazishi zitatolewa baadae.

Chanzo cha habari:Full shangwe

No comments:

Post a Comment