TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 14 March 2013

Offside Trick wameachia albam yao ya Nipe nikupe


 BAADA kukaa kimya kwa muda   hatimaye wasanii wakali wa mduara nchini offside trick  wamejitokeza na kusema walikuwa wanaandaa albam yao inayokuja kwa jina la Nipe Nikupe itakayokuwa  sokoni  kuanzia sasa.

Wakizungumza na safu hii, kundi hilo limesema kipindi chote ambacho walikuwa wametoweka sio kwamba walikuwa wamelala ila waliamua kufuata utaratibu wa jinsi ya kufanikisha albam yao na pia kuwasoma wapenzi wa muziki nini hasa wanataka ili wafanikishe hilo suala, na kwa upande mwingine kusoma makosa yao na kurekebesha pale ambapo wanahisi wanahitaji kuweka sawa.

“Tunajuwa kimya kimekuwa kikubwa na tunaelewa wapenzi wa mduara na wapenzi wa muziki kwa ujumla wana hamu sana kujua nini kinaendelea, tungependa kuwapeni habari nzuri kuwa kusubiri kwenu kumefikia mwisho,”wanasema.

Wanaeleza kuwa  waliamua kutafuta njia ya kuwezesha muziki wao  kuvuka mipaka na kufika kila kona ya ulimwengu ili  kuwapa wapenzi wao ladha tofauti  za dunia kuweza kupata nyimbo kwa urahisi.

Wanasema  album  hiyo  ya nipe nikupe  ambayo imekusanya  nyimbo zao zote zilizotamba  tayari imeshaingia sokoni na kwenye maduka ya online ikiwapo iTunes, Amazon Mp3, Spotify na mengineyo.

Kundi hilo linasema mwitikio wake  umekuwa   kinyume walivyokuwa wanategemea, kwani walipoamua kuingia kwenye soko hilo  hawakutarajia mauzo, ilikuwa  zaidi ni kutangaza mziki wao  wa kitanzania na kutengeneza  jina la Offside Trick  duniani.

Aidha, wamewaomba mashabiki wao kuwaunga mkono kwa kununua kazi zao.
Ladha ya nyimbo ni kama kawaida ile ile ya mduara ila wamejaribu kupiga hatua moja mbele ili kutowafanya wapenzi wachoke na kuwafanya kuhisi kuwa hakuna mpya.

Album ya Nipe nikupe  ina nyimbo nane ambazo ni  Chatu,  Nipe Nikupe, Kiwembe Feat H-Baba,  Usinipe  Feat Baby J,  Harusi Helwa Feat Zinho,  Talaka Feat Ommy,  Nipe Nikupe (remix) na  Babu jinga 


No comments:

Post a Comment