TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 5 April 2013

Kash Kash waamua kuuza CD zao wenyewe


Mchekeshaji maarufu wa runinga  nchini Habibu Mrisho aka Sumaku amesema kundi lake la Kashi kash limeamua  kufanya ziara katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuuza CD zao za vishekesho.

Akizungumza na blogu hii  jijini Dar es Salaam, Sumaku amesema ziara hiyo itaanza rasmi mwezi huu waApril, ambapo wataanza na mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na kwamba mashabiki wa vichekesho katika mikoa hiyo watafadika kwa vile wanatarajia kuuza CD zao kwa bei ambayo kila mtanzania anaweza kuimudu lengo ni kuwafurahisha wateja.

Baadhi ya wachekeshaji wa kash kash maarufu kama mizengwe
 Anasema wameamua kuuza CD zao wenyewe ili waweze kukusanya mapato mazuri yatakayowasaidia kufikia malengo waliyojiwekea, ya kuboresha kazi zao za kisanii na maisha kwa ujumla.

“Tumekuwa tukizunguka sehemu mbalimbali kuuza CD zetu na tunashukuru kwamba mashabiki wetu wanatupokea vizuri, tunauza wenyewe ili tupate kunufaika,”anasema.

Kundi la Kashi Kashi likiwa linaongozwa na Sumaku, limekuwa likifanya kazi na runinga ya ITV, ambapo wamekuwa wakivuma kwa umahiri wao kutunga stori za kuchekesha.

No comments:

Post a Comment