TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 9 April 2013

Kenyatta aapishwa kama Rais wa Kenya

Uhuru Kenyatta ameapishwa leo kama rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya kufuatia ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga katika uchaguzi uliofanyika Machi nne.

Ushindi wake wa kwanza katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, ulihalalishwa na mahakama ya juu zaidi nchini Kenya.

Maelfu ya wakenya walikusanyika katika uwanja wa michezo wa Kasarani viungani mwa mji wa Nairobi kushuhudia historia ambapo Kenyatta ameapishwa chini ya katiba mpya. 

No comments:

Post a Comment