TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 3 May 2013

Mwasiti afurahia kuchaguliwa tuzo za KilimanjaroMwasiti Almas
 MSANII mkali wa kike wa miondoko ya zuku nchini Mwasiti Almas amesema anajisikia faraja kuwa ni miongoni mwa wasanii, waliochaguliwa kupigiwa kura katika kategori 5 kwa ajili ya  kugombea tuzo za Kilimanjaro kwa mwaka 2013.

Katika majina ya wasanii waliochaguliwa kugombea tuzo hizo, Mwasiti anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na kategori nyingi ambapo anagombea tuzo ya wimbo bora wa mwaka kupitia wimbo wake wa Mapito.

Aidha, anagombea tuzo ya msanii bora wa kike, msanii bora wa kike bongo fleva, wimbo bora wa kushirikiana Mapito na wimbo bora wa zuku.

Akizungumza na safu hii, alisema tuzo hizo zimempa changamoto kwa kuona kuwa muziki wake unakubalika. Akaongeza kuwa anamshukuru Mungu kwani kuchaguliwa kwake kugombea tuzo nyingi imempa faraja ya kuendelea na muziki kwa kujiamini.

Hata hivyo, wasanii wanaoongoza kwa kugombea tuzo nyingi nafasi ya kwanza inashikwa na Ommy Dimpozi akigombea kategori 6 na nafasi ya pili inashikwa na Ben paul anagombea nafasi 5.

Katika hatua nyingine, msanii huyo alisema anatarajia kutambulisha ngoma yake mpya itakayotamba kwa jina la Wengine wiki hii yaani (wiki ijayo), ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wanaopenda muziki wake

No comments:

Post a Comment