TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 16 May 2013

Na Gazeti la Mwananchi:Ripoti ya Elimu bungeni yaibua utata

Dk Shukuru Kawambwa,Mwenyekiti (Waziri wa Elimu) picha na MwananchiKauli ya Serikali iliyotolewa bungeni juu ya kufutwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na sababu za kufeli kwa wanafunzi wengi, imeibua utata baada ya taarifa kadhaa kuonyesha kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilibariki mabadiliko ya mfumo mpya wa kupanga madaraja.

Taarifa ya Serikali iliyosomwa bungeni Mei 3, mwaka huu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi ilisema Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), lilifanya mabadiliko ya mfumo bila kushirikisha wadau.
“Baraza la Taifa la Mitihani lilikuwa linachakata alama za mwisho kwa kutumia mfumo ambao ulikuwa unabadilika kwa kutegemeana na hali ya ufaulu wa mwanafunzi... lakini mwaka 2012 lilitumia mfumo mpya wa kuwa na viwango maalumu vya kutunuku (fixed grade ranges).”
“Tume imebaini kwamba, pamoja na mfumo huo kuandaliwa kwa nia nzuri, utaratibu huo mpya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.
“Baraza la Taifa la Mitihani limeelekezwa kuzingatia kuwa pamoja na kwamba sheria ya kuanzishwa kwake inawaruhusu kufanya marekebisho ya mchakato wa mtihani, lakini marekebisho yoyote ya kubadilisha utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya matokeo ya mtihani lazima yahusishe wadau wote wanaohusika na mitalaa, ufundishaji na mitihani.”
Kwa mujibu wa vielelezo vilivyochapishwa na Gazeti la Wiki la Jamhuri, mfumo huo ulipitishwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa, kikao kilichokutana na kujadili mapendekezo ya Necta ya kubadili mfumo huo kiliongozwa na Waziri wa Elimu, Dk Shukuru Kawambwa na Katibu wake alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo.
Muhtasari wa kikao hicho unaonyesha wajumbe wa mkutano huo walikuwa ni pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba, Kamishna wa Elimu,  Profesa Eustell Bhalalusesa, Paulina K Mkonongo, Marystella Wassena, T.E. Temu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), Dk Primus Nkwera, Bunyanzu Ntmabi, H.A Lihawa wote wakiwa wajumbe kwa upande wa Wizara.

Kutoka Necta wajumbe walikuwa ni Dk C.E Msonde, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako, Mwenyekiti wa Bodi ya Necta, Profesa Rwekaza Mukandara pamoja na Profesa Sifuni Mchome, ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Aidha, Gesimba alimwandikia barua Katibu Mtendaji wa Necta yenye kumbukumbu namba CAC.109/437/01N Desemba 12 mwaka jana akiliagiza kutumia mfumo mpya wa kukokotoa alama za mitihani ya kidato cha nne na sita.
“Tafadhali rejea kikao kilichofanyika tarehe 10/12/2012 katika ukumbi wa mikutano wa wizara kuhusu somo tajwa hapo juu (Maagizo ya kuhusu utaratibu wa matumizi ya viwango vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha nne na sita).
“Viwango vya ufaulu vilivyopendekezwa na Baraza la Mitihani la Tanzania vitumike kwa mitihani ya Kidato cha Nne 2012 na Kidato cha Sita kwa mwaka 2012 tu.

No comments:

Post a Comment