TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 6 June 2013

Redds Miss Sinza kufanyika leo, Twanga kutambulisha nyimbo mpya

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga akizungumza na warembo
Na Mwandishi Wetu
Nani kutwaa taji la Redds Miss Sinza leo? Jibu la swali hilo litajulikana leo wakati warembo 12 wanaowania taji la hilo watakapopanda jukwaani kwenye ukumbi wa Meeda Club kushindania taji hilo.

Mashindano hayo ambayo yamepangwa kuanza saa 1.00 usiku, yatashuhudia Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred akivua taji lake la kwanza katika usiku huo ambao utakuwa na buudani za kila aina. Mbali ya kuwa Miss Sinza, Brigitte  pia anashikilia taji la Redds Miss Tanzania.

Mbunifu wa mitindo anayekuja juu kwa kasi, Veronica Lugenzi atanogesha shindano hilo kwa kuwavalisha nguo za mitindo mbali mbali warembo. Veronica ni mmoja wa wabunifu maarufu wa mitindo na ameahidi kuwapendezesha warembo wote katika usiku huo wa burudani.
Warembo wataanza kwa kucheza shoo ya ufunguzi na baadaye kupita jukwaani wakiwa wamevalia mavazi ya ubunifu, ufukweni na baadaye usiku kabla ya kujibu maswali kwa watakao ingia tano bora.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema jana kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na bendi  namba moja nchini, African Stars “wana Twanga Pepeta’ itatumbuiza siku kwa mara ya kwanza na kutoa zawadi kwa wakazi wa Sinza na vitongoji vyake.
Majuto alisema kuwa bendi hiyo itatambulisha nyimbo mpya ambazo zitatambulishwa rasmi katika uzinduzi uliopangwa kufanyika Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club.

“Ikumbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na wameandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto.
Alisema kuwa nyimbo mpya kama  Nyumbani ni Nyumbani, Ngumu Kumeza,  Shamba la Twanga  na nyimbo nyingine nyingi zitatambulishwa katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment