TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday 2 June 2013

NSSF All Media Stars yavunja rekodi ya Bunge FC, Yaichapa bao 1-0

Kombe hilo likiandaliwa kwa ajili ya kukabidhiwa NSSF ALL STARS
Kikosi cha wanahabari

Kikosi cha wanahabari na Wabunge



Na Mwandishi wetu
TIMU inayoundwa na wachezaji kutoka vyombo vya habari mbali mbali vilivyoshiriki katika michuano ya NSSF “NSSF Media All Stars” imevunja mwiko wa timu ya Bunge FC ya kutofungwa kwa miaka tisa baada ya kuichapa kwa bao 1-0.

Katika mchezo huo uliofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri na kuhudhuriwa na watazamaji wengi katika historia ya uwanja wa Jamhuri, ulikuwa mkali na wa kusisimua na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
NSSF all Media ilianza mchezo huo kwa kasi kufanya mashambulizi makali katika dakika 10 za kwanza. 

Julius Kihampa alikosa bao la wazi katika dakika ya pili baada  ya pasi safi kutoka kwa Mbozi Katala ambaye alishirikiana vyema na Maulid Kitenge, Wilbert Molandi na Emmanuel China.

Dakika ya saba, shuti la faulo iliyopigwa na nahodha wa timu hiyo, Majuto “Ronaldo” Omary iligonga mwamba baada ya kumshinda kipa wa Bunge FC Idd Azzan ambaye hakuweza kufanya lolote.


NSSF all Media ilisheherekea bao lake pekee katika dakika ya tisa kwa kichwa kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Majuto ambaye aliwatoka walinzi wawili kutoka upande wa kulia na kupiga krosi safi.

 Bunge FC ilijikuta ikiutafuta mpira kwa tochi muda mwingi, ilishindwa kufanya mashambulizi ya kina karibu  dakika 70 na kuifanya NSSF all Media Stars iliyokuwa chini ya kocha wake, mchezaji wa zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga,  Sanifu Lazaro ilitawala muda mwingi.

Baada ya goli hilo Bunge FC walijitahidi kushambulia lakini ngome ya NSSF Media Cup Stars FC chini ya kipa Said Ambua ilikuwa imara kuokoa hatari zote langoni.

Katika mechi ya wanawake, Bunge Quuens iliyokuwa ikiongozwa na Halima Mdee (GK) na Esta Bulaya (WD) ilitoka kifua mbele kwa magoli 31 kwa 18 ya NSSF Media Cup Stars Queens.

Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mawaziri mbalimbali pamoja na huku  mgeni rasmi akiwa   Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai,  Bunge Queens ilikuwa ikiongoza kwa magoli 17-10.

Magoli ya NSSF Media Cup Stars Queens yalifungwa na Lulu Habib na Imani Makongoro (GS) aliyemtoa jasho halima Mdee (GK).

Baada ya mechi hiyo Naibu Spika, Job Ndugai  alizipongeza timu za kombaini za NSSF hasa ya soka ambayo imeweka rekodi mpya kwa kuwafunga wabunge kwenye uwanja wao.

“ Mmeonyesha uwezo mzuri lakini pia mmeonyesha kweli nyie ni wachezaji makini kwani mara kwa mara wabunge hawafungwi hapa Dodoma lakini nyinyi mmekuwa wa kwanza hongereni sana," alisema Ndungai ambaye ndiye alikabidhi vikombe kwa washindi kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhan Dau.

No comments:

Post a Comment