TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 19 July 2013

EAC, sekta binafsi na vyama vya kiraia kukutana Nairobi

Na Mwandishi wa EANA
Kenya imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa Katibu Mkuu wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu masuala ya sekta binafsi na vyama vya kiraia utakaofanyika kati ya Oktoba 14 hadi 16, mjini Nairobi.

 Uamuzi huo ni miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa siku tatu wa wataalamu juu ya utekelezaji wa majadiliano ya kiushauri kwa ajili ya sekta binafasi na vyama vya kiraia pamoja na wadau wengine wenye nia na mtangamano wa EAC, uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Kampala.

 Mkutano huo wa wataalamu pia umechagua kauli mbiu ya mwaka huu kuwa: ‘EAC tunayoitaka.Kulenga Mafanikio ya Haraka,’’ kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwa Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).


 Mkutano wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania kati ya Desemba 11 na 12, 2012.

 Mkutano huo unalenga kutoa jukwaa la majadiliano kati ya Katibu Mkuu wa EAC na sekta binafsi pamoja na vyama vya kiraia juu ya namna ya kuboresha mchakato wa mtangamano ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kikanda.

 Wataalamu pia walijadili juu ya hadidu za rejea kwa ajili ya Kamati za Kitaifa na Kikanda ikiwa ni pamoja na kujadili rasimu ya utendaji wa Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC.

 ''Lengo kuu la Jukwaa hilo ni kuruhusi wadau mbalimbali waliochaguliwa na EAC kushauriana na kufanyakazi kwa pamoja kufikia malengo ya Jumuiya na kukuza jumuiya yenye misingi kutoka kwa wananchi wenyewe,'' alisema Mary Makoffi, Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii EAC, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Jamii, Jesca Eriyo. 

 Aliongeza kwamba Kamati za Majadiliano ya Kikanda kwa ajili ya Mkutwano wa Pili, itakutana mwezi Septemba kuweka mambo sawa kabla ya mkutano wenyewe mwezi Oktoba, mwaka huu mjini Naitobi, Kenya.

 Mapema katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Mkutano, Ronah Serwadda ambaye ni  Kamishna katika Wizara ya Afrika Mashariki nchini Uganda, alisema kwamba Jukwa la Katibu Mkuu wa EAC, ni muhimu katika kuimarisha na kupanua mtangamano wa kikanda.


''Unawawezesha wadau kufanya majadiliano ya moja kwa moja na Mtendaji Mkuu wa EAC ili kusukuma mbele agenda ya mtangamano wa Kikanda,'' aliwaambia wataalumu kutoka nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi. SM/LC/NI

No comments:

Post a Comment