TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 12 July 2013

Mama wa Professa Jay kuzikwa Jumapili

Professa Jay kushoto akiwa na mama yake mzazi


MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini  Joseph Haule maarufu kama Professa Jay amesema mama yake mzazi anatarajiwa kuzikwa Kesho Jumapili kwenye makaburi ya Kinondoni.

Mama wa msanii huyo maarufu kama mama Majanjala alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi baada ya kugongwa na gari aina ya starlet wakati alipokuwa akivuka barabara katika eneo la Mbezi mwisho ambapo ndiko yaliyoko makazi ya Professa Jay.

Akizungumz  na gazeti hili, Professa Jay alisema mama yake alikuwa na utamaduni wa kutoka wakati wa usiku kwa ajili ya mazoezi  kwasababu  alikuwa akichoka mchana kutwa kutokana na kutofanya shughuli zozote.

 “Mama yangu alikuwa na utamaduni wa kutoka kila siku jioni kwa ajili ya kutembea tembea kama sehemu ya mazoezi, sasa juzi wakati anatoka ndipo alipogongwa,”alisema.

Alisema mara baada ya dereva wa gari hiyo ya starlet kumgonga mama yake Professa Jay, alimchukua na kwenda kuchukua PF3 na kumkimbiza katika hospitali ya Tumbi Kibaha kwa ajili ya matibabu lakini hakukaa muda mrefu akapoteza maisha.

Professa Jay alisema msiba upo nyumbani kwake Mbezi mwisho na shughuli zote zitafanyika kwake, kisha mama yake huyo kuzikwa Jumapili.

Mama huyo aliwahi kufanya kazi kwenye Benki ya Posta Tanzania kama mtawala (administrator) ambapo alistaafu rasmi mwaka 2010. 

Mungu ailaze roho ya mama Mwanjala mahali pema peponi  na tunawapa pole Professa Jay na ndugu zake kwa kufiwa na mama yao.

No comments:

Post a Comment