TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 23 August 2013

Matatizo ya Taifa yatolewa ufumbuzi wake

Mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa  Joseph Goliama (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani)

Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Urejesho wa Maadili ya Taifa (Taumata) iliyosajiriwa kwa usajiri namna S.A 18827, imesisistiza kuwa kurejea katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa nasio vinginevyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa ndugu Joseph Goliama alisema kutoka katika maadili mabaya na kuingia katika maadili mema ndio ufumbuzi wa matatizo ya Taifa kwa sasa.

Alisema kuwa makundi mbalimbali ya wananchi kuacha maadili mema ya Taifa ndio kumekuwa  msingi chanzo na kiini cha Taifa kupoteza Sauti moja ya kuisikiliza na mwelekeo mmoja wa kuufuata hali inayosababisha makundi mbalimbali ya wananchi kutokuwa na amani kutopendana na kutokuaminiana.

Goliama alisema kuwa maadili mabaya ambayo yanafanya Taifa kupoteza amani, umoja na mawasiliano ni pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi kuwaziana mabaya, kutazamiana mabaya, kuneneana maneno mabaya, kutendeana mabaya, kuonana kwa jicho baya,kuhusiana kwa uhusiano mbaya, kufanyiana maamuzi yasiyo ya haki na kusimamiana kwa misimamo isiyo ya haki.

Tunawashauri watanzania wa makundi yote kurudi katika maadili mema na kuacha maadili mabaya ambayo yanatishia ustawi na maendeleo ya Taifa letu alisema Goliama.

Alitoa mfano na kusema maadili mabaya ndio yametumbukiza mataifa mengi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo akawataka wananchi wa makundi yote kulinda na kutetea maadili mema ambayo yameifanya Tanzania kuitwa kisiwa cha amani.

Aliitaka serikali kuangalia uwezekano wakuyakutanisha makundi yote ya wananchi nakuyakalisha pamoja ili yakubaliane ni Taifa gani yanataka kulijenga litakalohakikishia kila kundi ustawi na maendeleo endelevu .

Akifafanua zaidi alisema wadau wa amani na umoja wa Taifa ni wananchi wa makundi yote yakiwemo makundi ya dini, vyama vya siasa, jinsia, rika, wafanyabiashara, wafugaji, wakulima, wafanya kazi ,Askari nakuyataka makundi hayo kupigania amani na umoja na haki ili Taifa liapate ustawi na maendeleo endelevu.

Goliama alimalizia kwa kuitaka serikali iishirikishe taasisi ya urejesho wa maadili ya Taifa katika majukum yake ya kutafuta amani ,umoja na mshikamano wa kitaifa

No comments:

Post a Comment