TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 12 August 2013

Push Mobile kumwaga vitz 4, pikipiki 12 Fiesta

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki  wa muziki hapa nchini.
Aliongeza kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment