TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 25 September 2013

Serikali kuanzisha Benki ya Vijana

SERIKALI ina mpango wa kuanzisha benki ya vijana amabyo itakuwa ikiwapatia mikopo nafuu  ili kuwawezesha  kujiajiri  wenyewe  ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.

Kauli  hiyo imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ,jijini  Dares Salaam.

Makamu  huyo wa Rais  alisema hayo kufutia chapisho hilo kuonesha kwamba  kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi miaka 35 kuwa ni watu milioni 15.6 sawa na asiliamia 34.7 ya watu wote nchini.
 
“ Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza uzalishaji na hatimaye kukuza uchumi  wa nchi na kupunguza umasikini ,” alisema Balozi Seif.

 Aliongeza kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo ya   Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya kuendeleza vijana.

“ Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina dhamira ya Kuimarisha viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha vijana kupata ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi za maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao,” alisisitiza.

 Aidha aliongeza  kwamba kupitia  chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine la wazee wenye umri wa  miaka 60 au zaidi amabo ni milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana na Sera  ya Wazee kundi  hilo  linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na huduma nyingine muhimu.

“Serikali  na wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali ya uchumi wan chi,” alisema.

 Balozi Seif alizita  Wizara ,Idara na Taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha sera zilizopo  na kutumia takwimu hizi katika kupanga mipango ya maendeleo.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk. Albina Chuwa alisema  chapisho hilo linaonesha kuwa umri  unaoanzia miaka 0 hadi 4  kuashiria kuwa kiwango cha  uzazi bado ni kikubwa.

 Alifafanua kuwa kwa kumujibu wa Utafiti wa  Mama na Mtoto wa mwaka 2010 kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa miaka 15hadi 49, hivyo  uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.

Naye Mwakilishi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia (UNFPA)Mariam Khan alisema chapisho hilo  litasaidia kujua iddai ya watu wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga  uzazi wa mpango na mipango mingineyo.

No comments:

Post a Comment