TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 12 September 2013

Ufadhili ligi daraja la kwanza

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga akiwa ameshika jezi ya Mbeya city hivi karibuni baada ya kukabidhiwa jezi mbali kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara


BODI ya Ligi kuu Tanzania bara imehimiza wadau mbalimbali wa soka nchini kujitokeza na kufadhili michuano ya ligi daraja la kwanza.

Michuano ya ligi daraja la kwanza inaanza rasmi Septemba 14 hadi mwishoni mwa mwezi Oktoba, mwaka huu katika viwanja mbalimbali huku kukiwa hakuna mfadhili yeyote aliyejitokeza kwa ajili ya kudhamini  mashindano hayo.

Mkurugenzi wa bodi hiyo, Silas Mwakibinga ameiambia blogu hii  kuwa timu nyingi zinazocheza ligi daraja la kwanza zinatoka kwenye mazingira magumu zikiwa hazina vifaa vya michezo huku pia kukiwa na gharama kubwa za uendeshaji wa mashindano .

Alisema kutokana na timu hizo kutokuwa na udhamini Bodi ndio hugharamika kununua vifaa vya michezo kama mipira, bendera na vingine muhimu.

“Tunawahimiza wadau mbalimbali kujitokeza na kudhamini mashindano ya ligi daraja la kwanza, zinahitaji kupata udhamini ili ziweze kutoka kwenye mazingira magumu,”alisema.

Alisema kwa sasa wako kwenye mazungumzo na Kampuni ya EAG kwa ajili ya kuwatafutia udhamini wa ligi hiyo.

Kwa mujibu wa Mwakibinga, lengo la kutafuta wadhamini ni kuhakikisha sio tu ligi hiyo inapewa vifaa bali pia zinapata nafasi ya kutangazwa ili kuweza kuwavutia wawekezaji watakaojitokeza kuwekeza kwenye soka la Tanzania.

“Nategemea msimu ujao ligi zetu za daraja la kwanza nazo zitanufaika kama mikakati yetu ya kupata wadhamini itafanikiwa,”alisema.

Halikadhalika, tayari ameshaanza mazungumzo na kampuni moja ya utangazaji nchini kwa ajili ya kununua haki za matangazo ili kurusha  ligi daraja la kwanza, na dili litakapofanikiwa ataeleza ni akina nani.


No comments:

Post a Comment