TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 27 September 2013

Wanasiasa watakiwa kuacha kauli zinazohatarisha usalama


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba akizungumza na waandishi wa habari


Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini

Na Mwandishi wetu
SERIKALI imeshtushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha amani na usalama wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.

Waziri Simba amesema kuwa kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa vilivyofanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani zimeishtua Serikali na zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii hususani wanawake, wazee, walemavu na watoto. 

Waziri Simba amesema kauli zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na “Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika” kauli hii inahitaji tafakari na kuhoji kwa makini inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo linaweza kuwafanya walete vurugu..

Amesema kuwa kauli hiyo na nyingine zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa vyama hivyo zinazowachochea wananchi kutotii na ni ishara ya  uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mikononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu. 

Aidha, Waziri Simba alisema jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema kuwa jamii ya Watanzania inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wa jamii ya Watanzania unahitaji amani, utulivu na usalama.

No comments:

Post a Comment