TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 26 September 2013

Wataalamu wa kimataifa kusaidia Kenya

Na Bbc Swahili
Wataalamu wa kuchunguza mauaji kutoka nchini Marekani na Uingereza wamejiunga na kikosi cha wataalamu nchini Kenya kudadisi hali katika jengo la Westgate.

Waziri wa maswala ya ndani na usalama Joseph Ole Lenku amesema kuwa wataalamu wa Kimataifa watasaidiana na wale wa Kenya kuchunguza jumba hilo na kusisitiza kuwa Kenya itaongoza shughuli hiyo.

Pia wataalamu kutoka Israel pamoja na wahandisi wa nchini humu watasaidia kuchunguza kilichosababisha sehemu ya jengo hilo kuporomoka pamoja kuwatambua watu waliohusika na shambulizi hilo.

Akiwahutubia waandishi wa habari katika eneo la shambulizi, Ole Lenku alisema kuwa jumba la West Gate limekabidhiwa kwa wakuu wa ujasusi kwa shughuli zaidi za udadisi.

Aliongeza kuwa idadi ya maiti walio ndani ya jengo hilo chini ya vifusi , haijulikani ingawa alisisita kama bado kuna maiti idadi yao ni ndogo sana.

Maafisa wataendesha shughuli ya kuondoa vifusi ili kuondoa miili iliyonaswa katika jengo hilo.

Jengo la Westgate lilitekwa na magaidi Jumamosi mchana huku wakiwaua watu kiholela na kuwateka baadhi.
Takriban watu 61 waliuawa na magaidi hao wakiwemo maafisa sita wa usalama huku washukiwa wengine 11 wakikamatwa.

Rais Kenyatta alifanya mkutano maalum na baraza la mawaziri kuhusu shambulizi hilo ili kudadisi hali itakayofuata.

No comments:

Post a Comment