TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 29 November 2013

Mbio za Serengeti Marathon kufanyika Desemba 4



Na Mwandishi wetu
KITUO cha michezo cha Serengeti kilichopo mkoani Simiyu kimeandaa mashindano ya mbio za Serengeti Marathon zitakazofanyika Desemba 4, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa mbio hizo zinazofahamika kama Serengeti Marathon Xavier Mhagama alisema mashindano hayo yatawashirikisha wanariadha mbalimbali pamoja na viongozi.

Alisema mgeni rasmi atakuwa ni Waziri Mkuu  Mizengo Pinda. Alisema  washiriki kutoka Tanzania, Kenya na Sweden watashiriki mbio kuanzia kilometa 42, 21 na 5.

Miongoni wa wanariadhara maarufu watakaoongoza mbio hizo ni Dikson Marwa na Fairuna Mohamed. 

Alisema kauli mbiu ya shindano hilo no kupiga vita ujangili wa wanyama hasa Tembo, Faru katika maeneo ya hifadhi ambapo ndipo kuna janga kubwa la mauji ya wanyama hao.

“Kauli mbiu hiyo imekuja wakati muafaka kwa kuwa na wanyama wengi wanauawa na majangili bila kujali kuwa utalii unakuza uchumi wan chi na unategemea uwepo wa wanyama hao,”alisema.

Alisema hadi sasa maandalizi yamefikia sehemu nzuri ikiwa ni pamoja na Kampuni mbalimbali kujitokeza kufadhili mashindano kama Kampuni  bia ya Serengeti, Qualirty Group, Shirika la Hifadhi ya dunia(WWF), Mfuko wa pensheni wa LAPF, Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Gruments reserves na Jaji Mark Bomani.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo itakuwa hivi kwa  km 42 atapata Sh. Milion 2.5, wa mbio za km 21 atapata Milioni 1.5 na mshindi wa tatu Milioni 1.

Alisema kwa kumaliza mashindano hayo kutakuwa na ujenzi wa kituo cha watoto walemavu wa ngozi.

Katika kufanikisha ujenzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Serengeti Jaji Mark Bomani alichangia fedha kiasi cha Sh. Milioni 2.5 kwa ajili ya ununuzi wa dawa walemavu wa ngozi, wakati Kampuni ya Serengeti ilichangia Sh. Milion 5 huku twiga Cement wakichangia mifuko 600 ya saruji.

No comments:

Post a Comment