TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 28 November 2013

Mtanzania Ang'ara Miss Earth Ufilipino

Mrembo wa Tanzania (wa pili kushoto)Clara Noor akiwa na warembo wengine katika shindano la Miss dunia linalofanyika nchini Phillipines.
Mrembo wa Tanzania (wa pili kushoto)Clara Noor akiwa na warembo wengine baada ya kushinda taji la fukwe ya Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
Mrembo wa Tanzania Clara Noor akiwa katika pozi.

Mwandishi wetu
Nyota ya mrembo wa Tanzania anayewania taji la Miss Earth, Clara Noor imeanza kung’ara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika taji la fukwe ya Pagudpud iliyopo nchini Phillipines.
 
Mbali ya kutwaa taji hilo, Clara pia ameibuka mshindi wa tatu katika taji la vazi la Taifa na kuzipiku nchi nyingine nyingi na kuzawadiwa medali ya shaba.
Katika mashindano ya tuzo maalum, jumla ya tuzo 11 zilikuwa zinagombaniwa na warembo 88 walikuwa wanawania mataji hayo ambayo zawadi zake zilitolewa na wadhamini hao.
Clara alionyesha uwezo mkubwa katika taji hilo na kuwa mwafrika wa kwanza kushinda katika historia.  Katika vazi la Taifa, Clara aliwavutia wengi na kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mrembo wa warembo kutoka Afrika Kusini, Ashanti Mbanga na kutoka Nigeria, Marie Miller ambao walishika nafasi ya kwanza nay a pili.
Muandaaji wa Miss Earth Tanzania, Maria sarungi Tsehai alisema kuwa ni faraja kubwa kwa Clara kuitangaza Tanzania kwa kupitia mataji hayo mawili kwani mbali ya jina lake, kinachotangazwa pia ni nchi.
“Amefanya vyema mpaka sasa, tunatarajia kuona anaendelea kufanya vizuri na kutuletea sifa, mpaka sasa anastahili pongezi,” alisema Maria ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications.
Alisema kuwa fainali ya mashindano hayo yatafanyika Desemba 7 kwenye ukumbi wa Versailles Palace, Alabang, Muntinlupa City na kurushwa live na vituo vya televisheni vya STAR World, ABS-CBN, Velvet, The Filipino Channel, Ustream na VenevisiĆ³n.

No comments:

Post a Comment