TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Saturday 9 November 2013

Raia wa kigeni anaswa na Mafuvu Burundi

Polisi nchini Burundi wanasema zaidi ya mafuvu 40 ya binadamu yamepatikana katika makao ya raia mmoja wa Italia anayefanya kazi nchini humo.

Giussepe Favaro alikamatwa mwezi uliopita baada ya mafuvu mawili yaliyonuiwa kusafirishwa kwa ndege kunaswa katika uwanja wa ndege nchini Burundi.
Kwa mujibu wa polisi mafuvu hayo yalinuiwa kusafirishwa hadi nchini Thailand.
Polisi hata hivyo hawajatoa taarifa zaidi na mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema watu wana shauku ya kutaka kujua mafuvu hayo yalitoka wapi na yalikua yatumike kivipi.

Kumekuwepo ripoti za sehemu za miili ya binadamu kutumika katika ushirikina hasa katika nchi jirani ya Tanzania,lakini haifahamiki kwanini mafuvu yaliyopatikana hapo awali yalikua yakipelekwa Thailand.

Bw Favaro amekua akiishi nchini Burundi kwa miaka kadhaa.

No comments:

Post a Comment