TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 26 November 2013

Solly Mahlangu kutumbuiza Tamasha la Krismas

msamaNa 
Mwandishi Wetu
WAKATI Tamasha la Krismas likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.

Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1).

Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda).

Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.

No comments:

Post a Comment