TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 26 November 2013

Waziri Nchimbi azindua mpango Mkakati wa kuboresha madawati ya Kijinsia na watoto ndani ya Jeshi la Polisi

PIX 1 
Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa Askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali pamoja na wakazi wa Temeke kabla ya kuzindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa Kuboresha Madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi.  PIX 2-1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikionyesha kitabu cha Mpango Mkakati wa miaka mitatu wa kuboresha madawati ya Kijinsia na Watoto ndani ya Jeshi la Polisi katika uzinduzi uliofanyika Kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, wapili kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi na Kushoto ni Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.  PIX 4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wasita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi wa Mashirika na Taasisi zisizo za Serikali  wakiwa katika picha ya pamoja. Watano kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema. KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment