TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 11 November 2013

Uteuzi mpya wa Rais KikweteTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
                                         
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Prof. Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO).

Rais pia amemteua Bwana Freddy Safiel Manongi kuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambaye hivi sasa ni kaimu Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Mweka na pia amemteua Prof. Audax Zephania Philip Mabula kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam  kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Uteuzi huu umeanza rasmi mwishoni mwa Mwezi Octoba mwaka huu.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.

11 Novemba, 2013

No comments:

Post a Comment