TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 13 December 2013

Bioteknolojia ni nyenzo ya kuboresha uchumi-SalulaNa Mwandishi wetu
 
Bioteknojia ya kisasa ni nyenzo mpya inayoweza kuboresha sekta mbali mbali za kiuchumi zikiwemo sekta za kilimo, mifugo misitu, uzalishaji viwandani,  na hifadhi ya mazingira.
 
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula Katika ufunguzi wa Warsha ya kufunga mradi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.

Bw.Salula amesema kuwa, lengo kuu la teknnolojia hii ni kukidhi haja mbali mbali za binadamu kama vile kuimarisha ubora wa mazao, kukidhi magonjwa, kupata mbegu za mazao yanayohimili ukame na kukuza uzalishaji.


Aidha, aliongeza kuwa, pamoja na faida za bioteknolojia ya kisasa, bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea kutokana na bioteknolojia hii ikiwa ni pamoja na  uzio yaani allergy, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani na  usugu katika matibabu ya magonjwa.

Alisisitiza kuwa, serikali imejiandaa kupunguza na kudhibiti athari hizi kutokana na sababu kuwa Tanzania, haiwezi kukwepa athari zinazoweza kutokea kutokana na  muingiliano wa kimataifa hususan utandawazi pamoja na mianya iliyopo katika mipaka na kuzingatia umuhimu wa matumizi ya biteknolijia ya kisasa katika nchi yetu.

"Si kweli kwamba Tanzania inakataa matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa bali tunadhibiti ili kuepuka madhara yatokanayo na bioteknolojia ya hiyo, Alisisitiza"

Bw. Salula alianisha kuwa Tanzania kama nchi nyingine ni muhimu ikawa na mfumo na vifaa vitakavyodhibiti bioteknolojia ya kisasa, ikiwa ni wanachama wa mkataba wa Cartagena Tanzania inatakiwa kuweka taratibu zitakazo hakikisha matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa.

Mradi huu ulikuwa na lengo la kujenga uwezo kwa sekta na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na bioteknolojia ya kisasa ambapo maabara za taasisi tano zilipatiwa vifaa vya kisasa vya kusaidia kutambua na kufanya tathmini ya usimamizi angalifu wa bidhaa za mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki.

Maabara zilizonufaika na msaada huo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Taasisi ya Utafiti na Kilimo - Zanzibar, Taasisi ya Utafiti na Kilimo - Mikocheni na Mamlaka ya Chakula na Madawa Tanzania.


EVELYN MKOKOI NA LULU MUSSA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
13/12/2013

No comments:

Post a Comment