TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday 20 December 2013

Mama Salma apokewa kwa shangwe baada ya kurudi na tuzo ya uongozi

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye ofisi yake iliyoko karibu na Ikulu mara baada ya kuwasili nchini akitokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu alikopokea tuzo ya uongozi huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuja kumpokea
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea maua kutoka kwa Mwenyekiti wa wake wa viongozi, Mke wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa William Lukuvi na Mwakilishi kutoka ofisi ya WAMA, mara baada ya kuwasili ofisini hapoakitokea Dubai kupokea Tuzo ya uongozi itolewayo na Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD)

Baadhi ya wananchi walioshiriki mapokezi ya Mama Salma wanaonekana wakimsikiliza wakati alipokuwa akiwahutubia katika viwanja vya WAMA
Kikundi cha ngoma za utamaduni kikiburudisha mara baada ya kuwasili Mama Salma
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha TUZO wananchi waliokusanyika katika viwanja vya WAMA kwa ajili ya kumpongeza baada ya kuwasili nchini.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

No comments:

Post a Comment