TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday, 17 December 2013

Mama Salma Kikwete akiwa kwenye mkutano wa wanawake kutoka Afrika

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network,Tareq Ahmed Nizami, mwandaaji mwenza wa Mkutano wa  Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, 'The Africa -Middle East-Asia' unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu (UAE). Mwandaaji mwingine wa mkutano huo ni Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD).

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa  wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika Dubai.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasilisha mada ya Elimu: Key to the Future of Women in Emerging Economies, kwenye mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika huko Dubai.


No comments:

Post a Comment