TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 12 December 2013

NEYMAR AANZA SAFARI YA KUWAPINDUA RONALDO, MESSI UFALME WA DUNIA

  Na Bin Zubery Blog
NYOTA wa Brazil, Neymar jana alianza kutanua mbawa zake Ulaya, baada ya kufunga mabao matatu ndani ya dakika 13 katika ushindi wa Barcelona ya Hispania wa 6-1 dhidi ya Celtic ya Scotland katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Kwa kufanya hivyo, Neymar ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga hat trick za haraka, yaani kufunga mabao matatu ndani ya muda mfupi katika michuano ya Ulaya.
Mungu niwezeshe zaidi; Neymar akimshukuru Mungu baada ya kukamilisjha hat trick ndani ya dakika 13 jana
Neymar akishangilia hat trick yake ya ndani ya dakika 13

Desemba 7, 2011 Bafetimbi Gomis wa Lyon aliweka rekodi ya hat trick ya mapema zaidi dhidi ya Dinamo Zagreb ndani ya dakika saba, akivunja rekodi ya Mike Newell wa Blackburn aliyetumia dakika tisa na Marco van Basten wa AC Milan aliyetumia dakika 11.
 
Desemba 7, mwaka jana Claudio Pizarro wa Bayern Munich naye aliingia katika orodha ya wachezaji waliofunga hat trick za mapema, akifunga mabao matatu dhidi ya Lille ya Ufaransa ndani ya dakika 15.
 
Barcelona jana licha ya kuwakosa Andres Iniesta aliyebaki benchi, Leo Messi ambaye bado majeruhi na Cesc Fabregas anayetumikia adhabu, iliichapa mabao 6-1 Celtic.
 
Neymar aliyeongoza safu ya ushambuliaji hakufanya makosa baada ya kufunga hat trick yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa dakika za 45, 48 na 58, wakati mabao mengine yalifungwa na Pique dakika ya saba, Pedro dakika ya 39, na Tello dakika ya 72. 
 
Je, huu ni mwanzo wa Mbrazil huyo kuwasha moto zaidi Ulaya kuelekea kuwa mfalme wa dunia, akiwapindua Ronaldo na Messi? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

No comments:

Post a Comment