TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 2 December 2013

Waziri Mkuu Thailand agoma kujiuzulu

  
 Na Bbc Swahili
 
Waziri Mkuu wa Thailand amepinga madai ya wapinzani ya kumtaka ajiuzulu.

Yingluck Shinawatra amesema yuko tayari kwa mazungumzo na waandamanaji wanaoipinga serikali yake, lakini ameonya kuwa madai ya kumtaka ajiuzulu ni kinyume cha katiba.

Bi Yingluck amesema polisi hawatatumia nguvu dhidi ya waandamanaji, huku maandamano hayo yakiingia wiki ya pili sasa. Waandamanaji wamelazimisha shule kadha kufungwa pamoja na vyuo na shughuli za biashara.

Lakini kuna waandamanaji wachache zaidi kuliko ilivyokuwa katika siku za karibuni, na mwandishi wa BBC anasema inaonekana waandamanaji hao hawana uwezo wa kuendelea mbele katika kampeni yao ya kutaka kumng'oa madarakani waziri mkuu Yingluck Shinawatra.

No comments:

Post a Comment