TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 23 January 2014

Abakwa kwa amri ya wazee wa kijiji India

Na Bbc Swahili
Mshukiwa wa kitendo cha ubakaji
 Polisi nchini India wamewakamata wanaume 13 waliohusishwa na genge la wanaume waliombaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi.
 Inadaiwa wanaume, hao walimbaka mwanamke huyo kufuatia amri ya wazee wa kijiji ambao wamejipa wenyewe mamlaka ya mahakama ya kitamaduni.

Msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu akiwa hali mahututi.

Inaarifiwa amri ya kumbaka mwanamke huyo ilitolewa na wazee wa kijiji ambao walipinga uhusiano wake na mwanamume kutoka katika jamii tofauti.

Hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha genge la wanaume kumkaba mwanamke nchini India.

Tangu kisa cha ubakaji wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 uliofanywa na genge la wanaume mjini Delhi mwaka 2012 , swala la ubakaji limekuwa likiangaziwa sana nchini India.

Hasira ya mamilioni ya watu iliyotokana na kisa hicho ilipelekea vyombo vya habari nchini India kuanza kuangazia tatizo hilo , swala ambalo wangi walihisi lilikuwa limepuuzwa kwa muda mrefu.

Serikali nayo ilianza kuweka sheria kali kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya wanawake.

Lakini utekelezwaji wa sheria hizo bado ni changamoto katika nchi ambayo ustawi wa kijamii unakuwa kwa kujikokota na ukosefu wa usawa likisalia kuwa tatizo jengine kubwa.

Wengi wameshangazwa kuwa katika kisa hiki, ubakaji umeamrishwa na kikundi cha wazee wa kijiji ambao wamejipa mamlaka kama viongozi wa kijamii.

No comments:

Post a Comment