TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday, 19 January 2014

BABU MHOLANZI AFAGILIA MABEKI YANGA NA KIPA DIDA, KUHUSU WASHAMBULIAJI…

Na Baraka Kizuguto, Antalya
BAADA ya sare ya 0-0 jana na KS Flamurtari inayoshiriki Ligi Kuu ya Albania jana viwanja vya Side Stars Complex Manavgat, Antalya, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm ameusifu ukuta wa timu yake ni imara.

Alisema vijana wake wamecheza vizuri mechi ya jana na kwa ujumla timu zote ziliweza kucheza kwa nafasi, lakini kwa umakini wa walinzi wa timu zote ndio maana milango ilikua migumu kufunguka.
Yanga SC jana 
“KS Flamurtari ni timu nzuri, awali hawakutegemea kama watapata ushindani mkali kutoka kwetu, lakini kadri mchezo ulivyokua ukiendelea walishangaa kuona tuna kikosi safi kilichokamilika,”.

 “Washambulaji wetu walipata nafasi kadhaa, lakini hawakuweza kuzitumia vizuri, hali kadhalika mlinda mlango wetu Dida aliweza kuokoa hatari nyingi kipindi cha pili kutoka kwa wapinzani wetu” alisema Hans.
Yanga imebakisha siku tano kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi ya Mabingwa, jana ikicheza mchezo wake tatu tangu iweke kambi nchini Uturuki.

Katika mechi za awali,  mabingwa hao wa Tanzania Bara, Yanga walishinda mbili dhidi ya Ankara Sekerspor mabao 3-0 kabla ya kuifunga Altay SK 2-0.

No comments:

Post a Comment