TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday, 19 January 2014

REAL YAUA 5-0 LA LIGA, CRISTIANO RONALDO, BALE NA BENZEMA NI BBC LA HATARI MADRID

NYOTA watatu wa Real Madrid wanaounda safu kali ya ushambuliaji iitwayo ‘BBC’ wameifanya timu yao izifikie kwa pointi Barcelona na Atletico Madrid kileleni mwa Liga kufuatia kufunga mabao katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Real Betis inayosuasua mkiani.
 
Nyota hao ‘Bale, Benzema, Cristiano’ umoja wao leo ulikuwa majanga mbele ya kocha wa zamani wa West Brom, Pepe Mel. 
 
Mwanasoka Bora wa dunia, Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 12, Bale akafunga la pili dakika ya 25, Benzema la tatu dakika ya 45, Di Maria la nne dakika ya 62 na Morata akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 90. 
 
Real sasa imefikisha pointi 50 za Barca na Atletico, lakini imecheza mechi moja zaidi, 20 dhidi ya washindani wake hao katika mbio za ubingwa msimu huu. Barca itakuwa mgeni wa Levante kesho na Atletico Madrid itaikaribisha Sevilla.
Cristiano Ronaldo ameendelea kusherehekea vyema tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia baada ya kufunga bao la kwanza la Real Madrid katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Real Betis

Stori na Binzubeiryblog

No comments:

Post a Comment