TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 16 January 2014

Man City yailamba Rovers FA 5 - 0

YATIMIZA MABAO 99 MSIMU MMOJA ENGLAND. MANCHESTER  City imeifumua mabao 5-0 Blackburn katika mchezo wa marudiano wa Kombe la FA Raundi ya Nne jana usiku England Uwanja wa Etihad. Mabao ya City yamefungwa na Alvaro Negredo mawili dakika za 45, 47, Edin Dzeko mawili pia dakika za 67 na 79 na Sergio Aguero dakika ya 73. 

City sasa imefikisha jumla ya mabao 99 iliyofungwa msimu huu na sasa watu wanasubiri kwa hamu kuona nani atafungwa bao la 100 katika mchezo ujao.
Chanzo: Bin Zubeiry

No comments:

Post a Comment