TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday 19 January 2014

Mwandishi wa BBC Komla Dumor aaga dunia

Mwandishi wa BBC Komla Dumor amefariki ghafla nyumbani kwake kutokana na mshtuko wa moyo.

Komla na Morgan Tsvangirai katika studio za BBC London
  Alikuwa na miaka 41 alipopata mauti yake.Komla Dumor ameelezewa kuwa miongoni mwa waandishi shupavu barani Afrika.

Rais wa Ghana John Dramani Mahama amemtaja marehemu kama zawadi ya Ghana ulimwenguni na kuongezea kuwa Ghana imempoteza mmoja wa wajumbe wake.

Komla hivi karibuni alikuwa anaongoza kipindi cha Runinga kinachozungumzia maswala ya Afrika baada ya kufanya kazi katika radio moja nchini Ghana na vilevile radio ya BBC.

Mhariri wa habari za ulimwengu Andrew Whitehead amemtaja kuwa mwadishi shupavu aliyekuwa na uhusiano mzuri na wasikilizaji.

Bbc Swahili

No comments:

Post a Comment