TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 13 February 2014

Arsenal 0-0 Manchester United

Mchezaji wa Arsenal akikabiliana na mchezaji wa Manchester United

Arsenal imepoteza nafasi ya kurejea tena kileleni mwa ligi kuu ya Premier, baada ya kutoka sare ya kutofungana bao lolote na Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates.

Vijana hao wa Arsene Wenger, walikuwa wakijaribu kufuta aibu waliopata wiki iliyopita wakati walipofungwa magoli 5-1 na Liverpoool nayo Manchester United, kwa upande wake ilikuwa ikijinasua baada ya kutoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na Fulham mwishoni mwa juma lililopita.

Licha ya kuwa mechi hiyo ilikosa ladha ya hadhi ya timu mbili kuu zinapocheza, pande hizo mbili zilipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Hata hivyo ilibidi timu hizo mbili kugawana alama moja kila moja na Sasa Arsenal imesalia katika nafasi ya pili na alama 56 alama moja tu nyuma ya Chelsea.

Aliyekuwa mchezaji wa Arsenal Robin Van Persie, nusura aifunge klabu yake ya zamani lakini juhudi zake zilizimwa na Wojciech Szczesny.

Olivier Giroud naye alipoteza nafasi nzuri zaidi ya Arsenal ya kufunga Man United.

Manchester United yasalia nafasi ya saba

Robin Van Persie
Kufuatia sare hiyo, kocha wa Manchester United United David Moyes ataendelea kusubiri muda mrefu zaidi kabla ya kuandikisha ushindi wake wa kwanza katika uwanja wa Emirates.

Wakati huo huo, hali mbaya ya anga ilisababisha mechi mbili za ligi kuu ya premir kuhairishwa jana usiku.

Mechi kati ya Manchester City na Everton ilihairishwa kutokana na upepo mkali ili hali mjini Everton, Polisi waliwashauri masimamizi wa klabu hiyo kuhairisha mechi yao na Cyrstal Palace kwa sababu jengo moja lililokuwa karibu na uwanja huo uliporomoka.

Chanzo.Bbc Swahili

No comments:

Post a Comment