TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 11 February 2014

Mteja wa NBC Kigoma aibuka kidedea droo kubwa ya Promosheni ya weka Upewe

 Meneja katika Kitengo cha Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Dorothea Mabonye akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Mteja wa benki hiyo, Mary Malifedha Popote kutoka Kigoma amejishindia gari jipya aina ya Suzuki Swift lenye thamani ya shs milioni 28. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Abdallah Hemedy, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa na Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow.
 Mkuu wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Musa Jallow (katikati) akizungumza katika hafla ya droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Gaudence Shawa,   Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Meneja wa Kanda w NBC, Rachel Mwalukasa.
Meneja wa Kanda wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (katikati) akizungumza na mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa NBC, Raymond Mutagahywa na Mkuu wa Kitengo cha Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe

No comments:

Post a Comment