TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 3 February 2014

Muigizaji Philip Seymour Hoffman afariki

Marafiki na waigizaji wenza wa mmoja wa waigizaji mahiri Hollywood na mshindi kwa tuzo ya Oscar- Philip Seymour Hoffman, wamekuwa wakitoa rambi rambi zao baada ya taarifa za kifo chake.

Philip Seymour Hoffman mwenye umri wa miaka 46, alipatikana akiwa ameaga dunia ndani ya nyumba yake usiku wa kuamkia leo.

Msemaji wa polisi alisema kuwa wachunguzi walipata karatasi ndogo mbili zikiwa na kinachosemekana kuwa Heroin.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, familia yake ilisema kuwa imeshtushwa sana na taarifa za kifo cha muigizaji huyo.

Polisi wanasema kuwa wanaamini muigizaji huyo alikuwa ametumia kiwango kikubwa cha dawa za kulevya.

John Hurt muigizaji Muingereza ambaye alishirikiana naye katika filamu, "Owning Mahowny" ya mwaka 2003 -- alitaja kifo chake kama hasara kubwa na jambo la kusikitisha kwa sekta ya uigizaji nchini Marekani.
Muigizaji mashuhuri Tom Hanks alimtaja Hoffman kama mwenye talanta kubwa.

Philip Seymour Hoffman alishinda tuzo ya Oscar ya muigizaji bora zaidi katika filamu ya mwaka 2005 kwa jina Capote. Pia aliteuliwa mara kadhaa kwa tuzo la muigizaji msaidizi bora zaidi.

Hoffman alikuwa anazungumzia sana tatizo lake la kutumia dawa za kulevya ikiwemo katika mahojiano na shirika la habari la CBS mnamo mwaka 2006, akisema kuwa alitumia vibaya kila alichoweza kukipata.

No comments:

Post a Comment