TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Sunday 2 March 2014

Pinto atetea nafasi yake

JUMA Abbas Pinto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) leo baada ya mpinzani wake George John Ishabairu kujitoa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam. 

George alitangaza kujitoa baada ya kufika ukumbini, akisema kwamba Mwajiri wake, Wizara ya Maji amemwambia ajitoe. 
Wanaume tumerudi; Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akipongezana na Katibu wake, Amir Mhando baada ya kutangazwa washindi mchana huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
Kamati mpya ya Utendaji ya TASWA

Pinto alipata kura 82 wakati 13 zilimkataa, na Egbert Mkoko ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 67 dhidi ya 32 za Mohammed Omary Masenga.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Wambura Mgoyo alimtaja Amir Mhando kushinda tena nafasi ya Ukatibu Mkuu baada ya kupata kura 93. Mhando hakuwa na mpinzani na kura mbili tu zilimkataa.

Nafasi ya Katibu Msaidizi imekwenda kwa Grace Aloyce Hoka aliyepata kura 65 dhidi ya 31 za Alfred Lucas Mapunda.

Mweka Hazina Msaidizi Zena Suleiman Chande amepata kura 55 dhidi ya 40 za Elius John Kambili, Mweka Hazina Shija Richard Shija 57 amepata kura 57 dhidi ya 38 za Mohamed Salim Mkangara.

Walioshinda nafasi za Ujumbe ni Ibrahim Mkomwa Bakari, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa na Urick Chacha Maginga.
 
Chanzo. BinZubeiryblog

No comments:

Post a Comment