TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 12 October 2015

Madam Ritha atoa tamko kuhusu ushindi wa Kayumba
 Kufuatia malalamiko ya ushindi wa mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka huu Kayumba Juma, jaji mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsena ametoa tamko.


Kayumba alishinda shindano hilo juzi ambapo alijinyakulia kitita cha Milioni 50 pamoja na mkataba wa kusimamiwa kazi zake za sanaa wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 10 kutoka Tip Top Connection.


Kayumba alishinda akiwa amemwacha mshindani mwenzake Nassib Fonabo ambae watu mbalimbali ndio wamekuwa wakilalamika kuwa ndie alietakiwa kuwa mshindi.


Akizungumzia sakata hilo Jaji Mkuu huyo alisema kuwa kwa kawaida kazi ya majaji inakuwa ni kuwachuja washiriki kutokea mikoani na hadi kufikia hatua ya tano bora ambapo kwa mwaka huu ilikuwa ni hatua ya sita bora kutokana na ushindani kuwa mkali zaidi.


Alisema kuwa ikishafikia hatua hiyo inabakia kuwa ni kazi ya wananchi kuchagua mshindi na ndicho kilichofanyika siku hiyo na kujikuta Kayumba akishinda.


Alisema kuwa siku ya mwisho majaji hawana kazi ya kuwachuja washindi kwa kuwa inakuwa wananchi kupitia kura zao ndio wenye jukumu hilo.


Aliongeza kuwa Kayumba hadi siku ya mwisho ya kupiga kura alipigiwa zaidi ya kura elfu 15 na hiyo ilitokana na zaidi uchezaji na uimbaji wake ambao uliwavuyia zaidi wapenzi wa muziki.


"Sisi kama majaji hatuna ushawishi siku ya mwisho na hiyo inakuwa ni kazi ya majaji na kwa ushindi huo wa Kayumba ni wapiga kura wenyewe na sasa sisi tunahusika vipi hapo" alisema Jaji huyo.


Aliongeza kuwa " hakuna uchakachuaji wowote kwa kuwa washiriki wakibakia wawili kazi inakuwa ni kwa mashabiki katika kuwachagua washiriki hao wawili na ni wao wenyewe ndio wanakuwa na mbinu za kuwavutia watu kupiga kura".

No comments:

Post a Comment