TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 23 April 2012

DOKII SASA AKIMBILIA KUIMBA SIASA


Msanii wa maigizo nchini ‘Dokiii’amesema kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika kuimba muziki wa siasa katika kampeni mbalimbaki  za Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kumuunga mkono mama yake ambaye ni Mwanachama wa Chama hicho.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Dokii alisema muziki wa bongo fleva ameuweka pembeni na kwamba atakuwa akiimba zaidi muziki wa siasa na kuigiza filamu mbalimbali.

“Kwa sasa nimeweka muziki pembeni unajua tena mama yangu ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa(Nec) nimeona  nimuunge mkono kuimba nyimbo za kampeni na zinazohusu CCM,”alisema.

Pamoja na kuimba nyimbo za siasa alisema nia yake sio kuja kugombea Ubunge baadaye bali amevutiwa mwenyewe na Chama hicho kwani atakuwa anatumia kipaji chake cha uimbaji kuelimisha jamii masuala ya siasa.

Alisema pia pamoja na kuimba muziki wa siasa pia anaendelea na harakati za kuigiza katika filamu na sasa tayari wameshatoa filamu mbili zinazoitwa ‘sista duu’ na ‘machepele’.

Alisema baada ya siku mbili filamu hizo zitakuwa sokoni hivyo mashabiki wake wasikate tamaa wataendelea kumuona katika filamu mbalimbali na kuomba wamuunge mkono kwa kununua kazi  hizo.

No comments:

Post a Comment