TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 23 April 2012

MCHEZAJI WA TWIGA STARS ALIYEJALIWA VIPAJI KIBAO


Anaitwa Semeni Abeid ni msichana mdogo aliyemaliza masomo yake mwaka jana Mkwakwani Tanga. Umri wake ni mdogo lakini mambo yake ni makubwa. Ni mchezaji ambaye anaweza michezo kama mitatu alikuwa akiimudu wakati yuko shuleni.

Wengi wanaofuatilia Twiga Stars huyu ni mchezaji ambaye anacheza namba tisa na vile vile ni mchezaji wa mpira wa kikapu katika timu ya Tanga United. Lakini pia anasema alikuwa anacheza Netball na michezo yote anaimudu.

Unapomuona uwanjani anachngamka na anajiamini kiasi kwamba aliwavutia watazamaji ambao walikuwepo katika mashindano ya kikapu ya ligi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Anasema anapenda sana michezo ndio maana alikuwa akishiriki yote na leo anachezea timu kubwa ya wanawake Tanzania. Kipaji chake kilianza kuonekana katika timu ya wanawake ya Tanzanite ambapo ndiko alikotokea hadi kufika Twiga Stars.

Malengo yake makubwa ni kuwa siku moja aje awe ni mchezaji wa kulipwa sio tu Tanzania hata kwa upande wa Kimataifa.

Anapogundua tatizo lake mapema anajipanga na kuhakikisha kwamba analifanyika kazi ili aweze kufanya vizuri zaidi.

No comments:

Post a Comment