Baada ya kimya cha takribani miaka miwili sasa
hatimaye Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Kabula George ameamua kurudi tena katika
sanaa ya muziki wa injili kwa kishindo kwa kutoa albam yake mpya inayobebwa na wimbo wa nitang’ara ikiwa
imebeba ujumbe wa kumsifu Mungu.
Mwimbaji huyo anayefahamika ndani na nje ya nchi
kutokana na uimbaji wake ameliambia gazeti hili kuwa wimbo wa nitang’ara
ukiwa pamoja na nyimbo nyingine sita
zimeanza kusikika katika redio mbalimbali, ila kwa upande wa video wameanza
mchakato wa kurekodi ambapo hadi mwishoni mwa mwezi huu itakuwa imekamilika.
Nyimbo sita zilizoko katika albam hiyo ni
Nitang’ara, Majaribu, Nimesogea, Nataka kumwona Yesu, Ni mwema na peleleza ambazo zote zimelenga kutoa elimu
kwa jamii hasa wale wanaomwamini Mungu na hata wasioamwamini Mungu wakisilikiza
watabarikiwa.
Anasema “Namshukuru Mungu
kwasababu nimefanikiwa kurekodi nyimbo zangu sita katika audio na sasa tuko
katika kurekodi video na nawaeleza mashabiki wa muziki wa injili kwamba
mwishoni mwa mwezi huu itakuwa sokoni hivyo naomba watuunge mkono katika
kumsifu Mungu,”.
Kabula anaelezea jinsi ambavyo
aliguswa kutunga wimbo wa
nitang’ara ambao ndio uliobeba
albam yake kwamba wimbo huu aliupata
baada ya kupitiaa katika maisha magumu yaliyosababisha baadhi ya majirani zake
kumbeza kutokana na changamoto alizokuwa
akizipitia .
“Nimepita katika nyumba
mbalimbali ambazo majirani walikuwa hawaishi kunibeza. Nikiwa katika hali ya
kuutafakari uweza wa Mungu kwa kuona kama ameniacha ndipo nilipopata wimbo
huu,”anasema Kabula.
Wimbo huo aliupata kutokana na
kuongeza juhudi za maombi kwa kuamini kuwa siku moja atang’ara licha ya kupita
katika changamoto hizo ambazo wamekuwa wakizipata watu mbalimbali hasa
wanaoishi kwenye nyumba za kupanga.
Anasema kuwa kupitia wimbo huo,
tayari kuna baadhi ya watu umewagusa kwa namna moja ama nyingine kwani
amekuwa akipata simu mbalimbali za kumpongeza
hasa ukizingatia kuwa ni wimbo
unaozungumzia maisha hivyo umewagusa wengi wanaokutana na changamoto za namna
hiyo, wanaamini siku moja watang’ara.
Historia
Kabula George alianza kuimba muziki
wa injili akiwa bado ni mtoto mdogo, mazingira aliyolelewa ya kumsifu
Mungu yalimfanya kuwa na moyo wa
kuendelea kuhudumia watu kupitia uimbaji.
Mwaka 2003 alijiunga na kwaya ya
Uinjilisti ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kinyerezi, ambapo
aliimba kwaya hadi mwaka 2005 alipoolewa na Mume wake George Kayala ndipo
alipoamua kurekodi ili kuendeleza huduma
hiyo.
Albam yake ya kwanza aliitoa
mwaka 2005 ilibebwa na wimbo wa Amani lakini kutokana na matatizo ya hapa na
pale akaelezwa kuwa haina ubora unaohitajika hivyo mwaka 2007 akurudia kurekodi tena huku akichukua baadhi
ya nyimbo na kuzirudia akabadilisha jina na kuiita ‘PESA’
Alibamu hiyo iliingia sokoni na
ilifanya vizuri wakati huo. Mwaka 2009
alifanikiwa kurekodi albamu ya pili iliyojulikana kwa jina la Ushindi. Ambapo
ndani yake kulikuwa na wimbo wa
dhihirisha ambao ulionekana kupendwa sana na watu na kumtambulisha katika anga
ya muziki wa injili.
No comments:
Post a Comment