TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 12 April 2012

MVUA ZA JANA ZASABABISHA MAAFA MTAA WA MISSION KIJICHI, MAITI ZA WATOTO ZAOKOLEWA

Mto wa Daraja la Kijichi umesababisha maafa makubwa kwa wakazi wa mtaa huo baada ya kujaa maji jana kutokana na mvua za jana na kuvamia nyumba za wakazi wa eneo hilo nyingi zimebomoka na nyingine kubomoka upande wakati nyingine zimejaa maji


Hapo unapoona ni nyuma imebomoka ambapo kuna mtoto mmoja alitolewa jana akiwa tayari ameshakufa baada ya nyumba kumbomokea, mtoto mwenzake apotezwa na maji haonekani na mama wa mtoto amevunjia mguu na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
 
Wakazi wa Mtaa wa Darajani wakishangaa nyumba zilizobomolewa na maji

Wakazi wa Mtaa wa Darajani wakishangaa
 
Hii ni nyumba iliyokumbwa na mafuriko

Hii nyumba imebomoka kwa mbele

Kundi la Vijana wa Mtaa wa Darajani Kijichi wakiwa wameokoa maiti ya mtoto wa darasa la saba aliyepoteza toka jana

Maiti ya mtoto wa miaka 7 iliyookolewa kutoka kwenye maji





Kundi la watu wa Mtaa wa Darajani Kijichi wakishangaa maiti za watoto zilizopakizwa katika gari la Polisi ili kwenda kuhifadhiwa Hospitalini




Kipande cha Barabara ya Mtoni Kijichi ikiwa nayo imeharibiwa vibaya kutokana na mvua hizo




Mkuu wa Mkoa wa Dar Sadick Meck Sadick katikati, kushoto kamanda Kova, Kulia ni Diwani wa kata ya Kijichi Charles na viongozi wengine walitembelea mtaa wa Darajani na kutoa pole huku akiagiza wapatiwe viwanja vilivyopimwa ili wahame mara




Mjumbe wa nyumba kumi Tosi Tosi akisema wako tayari kuhama iwapo watapewa viwanja

No comments:

Post a Comment